
TTaasisi ya wataalam wa masuala ya kuendeleza biashara Tanzania (TAPBDS CO. LTD) imepokea ruzuku kutoka kwa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) kwa kuongeza matumizi ya teknolojia za kupunguza hasara baada ya mavuno chini ya mradi unaoitwa âkuongeza kasi ya utumiaji wa teknolojia za kupunguza upoteaji wa mazao baada ya mavuno na kufanya mifumo ya chakula imara zaidiâ
MUHTASARI
Mlipuko wa ugonjwa wa korona (COVID-19) umeathiri mtiririko wa biashara ya chakula na kusababisha nchi nyingi kuhifadhi vyakula vyao. Hii inaweza kusababisha upatikanaji mdogo wa chakula katika nchi nyingi kama mlipuko wa ugonjwa utaendelea. Njia za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa korona (COVID-19) ni pamoja na udhibiti wa kuingia na kutoka kwa watu na bidhaa, kutokana na kujifungia na vizuizi vya safari. Vizuizi vya kuingia na kutoka kwa watu na bidhaa vinaweza kuzidisha ukosefu wa usalama wa chakula, kwani inasababisha:-
- Upungufu wa nguvu kazi kwenye kilimo (kwaajili ya uvunaji na usindikaji), kunafanya matumizi ya mitambo kuwa njia sahihi ya kuendelea na shughuli za kilimo na kufanya uhusishwaji mdogo wa binadamu.
- Kuongezeka kwa hasara baada ya mavuno kwakuwa mazao hubakia shambani wiki kadhaa zaidi ya kipindi cha kukomaa.
- Kuwepo kwa njia chache za kufikia masoko kwa wakulima wanaovuna, hivyo uhitaji wa kusindika na kuhifadhi ni salama, safi na inapatikana maeneo ya karibu.
Utumiaji wa mashine katika shughuli za Kilimo unapelekea uzalishaji wa hali ya juu wa shambani na nguvu kazi, na kuhakikisha kiasi kidogo cha chakula kinapote kutokana na upungufu wa ubora na wadudu.
Kupitia mradi huu tungependa kuendeleza mradi wa awali wa AGRA katika kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno nchini Tanzania ambapo teknolojia mbalimbali zimethibitika zinafaa kukuzwa zaidi. Kwa kuongeza kasi ya kuchukua na kutumia teknolojia iliyoboreshwa na iliyothibitishwa ya kuvuna, kupukuchua, kusindika, kuhifadhi na kusafirisha mazao kutoka shambani hadi sokoni, TAPBDS inatoa majibu dhidi ya vizuizi vinavyohusiana na ugonjwa wa korona (COVID19)
Tafadhali endelea kusoma zaidi kwa kupakua kitabu hapa chini.